Remix ya Number One ya Diamond Yamkutanisha na Director wa Alingo ya P Squire
Diamond anaweza kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kufanya video na director mkubwa wa Nigeria Clarence Peter ambaye ameshafanya video nyingi za wasanii wakubwa nchini Nigeria na Africa kwa ujumla.
Diamond ame-post picha moja ya behind the scene wakiwa wanatengeneza hiyo video na aliandika hii caption , “Naamini ipo siku nasi Tanzania tutasimama vyema katika ramani hii ya muziki worldwide na kuipa sifa na heshima zaidi East Africa yetu. Eeeh Mwenyezi Mungu ibariki Tanzani, ibariki East Africa na Africa yetu kwa ujumla. #LastNight #Onset #NumberOneRemix#DiamondFtDavido #ClarencePeterBehindTheCamera”