Snura Kupamba Finali za EBSS Leo
MAMA wa Majanga, Snura Mushi leo anadondoka katika Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar katika fainali za Shindano la Epic Bongo Star Search.
Kwenye fainali hizo ambazo mshindi anatarajiwa kuondoka na kitita cha Sh. Mil. 50, wasanii mbalimbali wanatarajia kutumbuiza akiwemo Barnaba, Young Killer, Shaah, Msechu na Walter Chilambo.
Akizungumzia viingilio, jaji mkuu wa shindano hilo, Rita Paulsen ‘Madam’,alisema kuwa kutakuwa na vitu maalum kwa Sh: 50,000 ambapo watapata na vinywaji na pia kutakuwa na viti vya kawaida 20,000 na tiketi zinapatikana Shear Illusion ya Mlimani City, Best Bites, Steers ya mjini na Zizzou Fashion ya Victoria na Sinza Africa Sana pamoja na Escape One.
Madam alisema mshindi atakayepatikana leo atakuwa akisimamiwa na studio ya MJ na kufanyiwa kila kitu kwa sababu washindi wengi wanapopata fedha wanajali kufanya vitu vingine kuliko kuendeleza vipaji vyao.