Watu 6 Mbaroni kwa Tuhuma za Kumshambulia Dkt Sengondo Mvungi


 WATU 6 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuhusika na tukio la kumshambulia Dkt. Sengondo Mvungi aliyevamiwa na majambazi nyumbani kwake Kibamba Msakuzi juzi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Selemani Kova amesema katika operesheni maalum iliyofanywa na jeshi la polisi, wamefanikiwa kuwakamata watu sita ambao majina yako yamehifadhiwa kwa sababu za usalama.

Aidha Kamanda Kova aliongeeza kuwa bado hawajapata uthibitisho kamili juu ya sakata hilo na uchunguzi unaendelea kuwabaini wahusika halisi wa shambulio hilo

GPL.

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger