Baada ya Miaka 80 ya kuishi pamoja, wafunga pingu za Maisha.
Kisa chao cha Map3nzi kilianza miaka 6 kabla ya kutokea vita ya pili ya dunia, mpaka sasa imepita miaka 80 (Themanini )tangu Wap3nzi hao wakutane na kupendana na hatimaye kuanza kuishi pamoja mnamo mwaka 1933.
Jose Manuel Riella, 103 alichukua kiapo cha ndoa kwa mkewe Bi Martina Lopez, 99 wote raia kutoka Paraguay katika sherehe iliyohudhuriwa na wanandugu. Mpaka sasa wanandoa hao wamejaaliwa kupata watoto 8, wajukuu 50, vitukuu 35 na vining'ina 20.
Mchungaji aliyewafungisha ndoa hiyo ya kanisani amekiri kuwa katika maisha yake yote hajawahi kufungisha ndoa mpya ya watu wenye umri mkubwa kama huo. Awali wawili hao walifunga ndoa ya Kiserikali miaka 31 iliyopita lakini wameona muda umefika wafanye ndoa ya ki imani zaidi,