BAADA YA MBURUNDI KUSHINDA TUSKER PROJECT FAME SHANGWE ZA KWAO ZIMEKUWA HIVI
Pengine hii itakuwa ni mara ya kwanza na historia kwa nchi hiyo kutoa mshindi katika mashindano makubwa kama haya, huko pande za kwao kumekuwa na furaha na shangwe zisizo na kifani kutoka kwa raia wa nchi hiyo.
Mshiriki Hope toka Burundi amejikuta akianguka chini kwa mshituko wa furaha ulimkuta baada ya kuibuka kidedea kwa kutangazwa mshindi wa Tusker Project Fame na kujinyakulia kitita cha Shilingi 5,000,000/= za Kenya .
Mashindano hayo yaliyomalizika hivi punde usiku wa jana yamemwacha Hope katika taharuki huku akiwabwaga wenziye; Hisia (Tanzania), Patrick (Rwanda),Wambura (Kenya), Daisy (Uganda),Amos & Josh wa Kenya