Lina asaka Mimba




Akizungumza na  mwandishi wetu Desemba 9, mwaka huu jijini Dar, Linah alisema tangu alipoingia kwenye muziki hakuwahi kufikiria kushika ujauzito kwa kuwa alikuwa bado hajajiandaa kufanya hivyo.
Nyota huyo ambaye aliwahi kuzama  katika penzi zito la  staa mwenzake, Amin Mwinyimkuu alisema kuwa kwa sasa hali ni tofauti na anataka kuzaa iwapo atashika ujauzito.

“Nilipokuwa  katika uhusiano wangu wa kwanza hakuna hata siku moja niliyohisi kama nitakuja kutamani kupata mtoto maana mwenzangu aliponiambia tuzae nilimkatalia tofauti na leo hii natamani nishike mimba na ulimwengu wote ujue kwamba nina mimba,” alisema Linah.
Hata hivyo Linah alikwepa kuweka wazi uhusiano wake wa sasa na hakutaka kumwongelea Amin.
Views: 850

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger