MZEE SMALL YUPO HAI, AKANUSHA UVUMI WA KIFO CHAKE ULIOENEA MITAANI
KUNA taarifa zilizagaa kuwa msanii mkongwe wa vichekesho na maigizo nchini, Said Ngamba ‘Mzee Small’ amefariki dunia. Taarifa hizo ni za uongo na uzushi maana mwandishi wetu ameongea na mke wa Mzee Small pamoja na Mzee Small mwenyewe ambaye ni mzima kabisa! Mke wa Mzee Small anadai usiku kucha hajalala maana alikuwa anapokea meseji za pole kutoka kwa watu mbalimbali kuhusu taarifa hizo za uzushi. Mzee Small mwenyewe amesema: "Mimi ni mzima kabisa japo bado nasumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi (stroke)"