MAWAKILI WA ZITTO KABWE WAITISHA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI LEO HII
MWANASHERIA wa Mhe Zitto Zuberi Kabwe (Mb), Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, Ndugu Albert Msando, atazungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika Hoteli ya Serena leo tarehe 11/12/2013 kuanzia saa nne na nusu asubuhi (saa 4.30 asubuhi)
Dhima ya mkutano huu itakuwa kutoa ufafafunuzi juu ya mashitaka 11 na majibu yake ambayo Mhe. Zitto Kabwe na washitakiwa wenzake walipewa na Kamati Kuu ya CHADEMA. Aidha, katika kikao hiki Ndugu Msando, kwa niaba ya wateja wake, ataeleza hatua ambazo wateja wake wanazichukua ndani ya chama katika kuhakikisha kwamba mgogoro uliopo unakwisha kwa amani na haraka iwezekanavyo bila kuleta athari zaidi kwa chama.
Tunatanguliza shukrani na tunaomba waalikwa wazingatie muda.
Imetolewa na Ofisi ya Mbunge Zitto Kabwe,
Jumanne, 10 Desemba 2013
Dar es Salaam