NAY WA MITEGO ABAMBWA AKIWA NA LUNDO LA MABINTI, MANAIKI STYLE.



MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, amefungua ukurasa mpya wa skendo baada  kuachia picha zake alizozipiga kihasarahara akiwa laivu na warembo katika chumba cha hoteli moja maarufu jijini Nairobi nchini Kenya.
Nay wa Mitego akiwpozi na warembo katika chumba cha hoteli moja maarufu jijini Nairobi nchini Kenya.
Mkali huyo ambaye anatamba na kibao ha Peleka Salam, amevujisha picha hizo zinazomuonesha akiwa amezungukwa na warembo hao huku sehemu  kubwa ya mwili wake ukiwa wazi  na nyingine kufunikwa na taulo.
Nay akiwa amezungukwa na warembo.
Aidha warembo hao nao walionekana kuchojoa viwalo vyao na kujifunika mataulo tu kuziba sehemu za miili yao.
Nay wa Mitegho ambaye alienda Nairobi hivi karibuni na kukutana na wasanii kadhaa wa  jijini humo ambao walimtembeza  katika viwanja kadhaa vya starehe katika mishemishe  za kujirusha na kugundua kwamba anakubalika sana nchini humo.
...Akichat kwenye simu katikati ya warembo hao.
Mwandishi wetu alimvutia waya, Nay wa Mitego ambaye amerejea nchini hivi karibuni ili kutaka kujua  sababu za kupiga picha hizo , msanii huyo alikiri kuzipiga huku akikanusha kutenda ufuska wa aina yoyote ile.
...Mtu kati
“ Nilipokuwa Nairobi nimepiga picha nyingi kutokana na kuwa  na mashabiki wengi nchini humo  lakini zipo nyingine ambazo kwa kweli si nzuri ila nilizipiga kwa ajili ya video yangu mpya,” alisema Nay wa Mitego.”

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger