MSANII WA FM ACADEMIA AFANYIWA KITU MBAYA NA MADEREVA BAJAJ ALIOWAKODI BAADA YA KULEWA



DUNIA kweli haina huruma! Kitendo alichofanyiwa  mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia ya jijini Dar  anayejulikana kwa jina moja la Flora alfajiri ya kuamkia Desemba 8, mwaka huu ni kibaya katika jamii ya Kitanzania.
Flora akiwa hajitambui.
Flora akiwa amepata kinywaji ili kuchangamsha mwili wake alijikuta akipigwa na vijana wawili wanaofanya kazi ya kuendesha Bajaj akiwa amewakodi kwa ajili ya kurudi nyumbani  kwake.
Wananchi wakipanga jinsi ya kumsaidia Flora.
Tukio  hilo lilitokea maeneo ya Mwananyamala jirani na MK Pub jijini jirani kabisa na ofisi ya Msanii Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ limeacha simanzi kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.
Mmoja wa wananchi akijaribu kumnyanyua Flora.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu inadaiwa kuwa, Flora alipigwa na vijana hao na kuporwa  vitu vyake vya thamani ikiwemo simu pamoja na pochi lililokuwa na kiasi cha fedha ambavyo vyote bado havijajulikana  thamani yake.
Mbali na kumpiga,  vijana hao waliokuwa waliokuwa wakisaidiana kufanya kazi katika Bajaji hiyo wanadaiwa kumvua nguo mwanamuziki huyo ambaye aliwahi kutunga na kuimba kibao cha Sintasahau huku akishiriki kuimba vibao vingine vya FM Academia kama vile Dunia Kigeugeu, Shida  na Heshima kwa Wanawake.
“Tulikuwa tumekaa naye hapa tukila chips (MK) baada ya kumaliza kula Flora alionekana akikodi Bajaj ili kurudi  nyumbani kwake, baada ya muda tukawaona watu wakikimbilia kule kwenye ofisi ya Chuz, tulipoenda tukamkuta Flora akipewa msaada na mlinzi  na mwanamuziki mwingine kutokana na unyama aliofanyiwa,” alisema shuhuda  huyo.
Naye mlinzi aliyekutwa eneo la tukio alipoulizwa kuhusina jinsi kitendo hicho kilivyotokea, alisema kuwa aliiona Bajaj ikisimama eneo hilo na watu wanne wakashuka akiwemo Flora na baada ya muda kidogo alimuona mtu akijikokota alipomsogelea ndipo alipomuona  mwanamuziki huyo akiwa amevuliwa nguo.
“Wamemfanyia unyama sana wale vijana, sijui nini kingetokea kama ningegundua kabla hawajatenda unyama wao,” alisema mlinzi huyo aliyekataa kutajwa jina lake gazetini.
Flora aliondolewa eneo hilo baada ya kupewa msaada wa nguo na mmoja wa majirani wa eneo hilo ili ajisitiri.
Baada  ya tukio hilo, mwandishi wetu alimpigia simu Kiongozi wa FM Academia, Nyoshi El Sadaat lakini hakuweza kupokea ndipo akahamia kwa mwanamuziki wa bendi hiyo, Patcho Mwamba na kumuuliza kama Flora bado yuko FM Academia.
Patcho alikiri uwepo wa Flora katika bendi yao lakini alisema kwamba siku hizi mbilI hajaonekana na alisikitika alipopewa kisanga hicho kilichomkuta.
“Ni kweli tunaye Flora lakini siku hizi mbili hakuwepo kazini dah! Wamemfanyia unyama sana, madereva  wengine wa Bajaj si watu wazuri,“ alisema Patcho.
Mpaka sasa haijajulikana kama

GPL


Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger