MWANAMITINDO NAOMI CAMPBELL AMWAGA MACHOZI MBELE YA JENEZA LA MANDELA
Mwanamitindo nyota Duniani Naomi Campbell alijikuta akimwaga machozi alipokuwa anapita kuliangalia jeneza la Hayati Nelson Mandela, wakati mwili wa nembo ya mpigania ubaguzi wa rangi huyo na aliyekuwa Rais mweusi wa kwanza wa Afrika Kusini ulipowekwa kwenye majengo ya Union ndani jiji la Pretoria.
Maelfu ya watu walifika kumuaga Mandela, watu mashuhuri Duniani walitoa heshima zao za mwisho kwa nembo hiyo ya Ulimwengu.
Nelson Mandela alifariki mnamo Alhamisi ya December 5, 2013 akiwa na umri wa miaka 95 na atazikwa siku ya Jumapili December 15, 2013 ndani ya Qunu, nyumbani kwao Mashariki ya Jimbo la Cape.