ZAHA AKANUSHA KUWA NA MAHUSIANO NA MTOTO WA KOCHA WAKE, ASISITIZA HIYO SI SABABU YA KUKOSA NAMBA MAN U.





Wilfried Zaha amechukua hatua ya aina yake kukanusha taarifa zilizozagaa kwamba ana uhusiano wa kmap3nzi na mtoto wa kike wa kocha mkuu wa Manchester United David Moyes.
Winga huyo mwenye miaka 21 alinunuliwa na Sir Alex Ferguson kwa £15milllion lakini ameshindwa kupata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha kwanza chini ya David Moyes.
Kumekuwepo na taarifa kwamba amekuwa hapewi nafasi ya kucheza na Moyes kwasababu ya mahusiano yake na binti wa kocha huyo aitwaye Lauren.
Lakini Zaha - ameonekana kukerwa sana na tetesi hizo - ametumia ukurasa wake wa Twittet kuwaambia mashabiki 490,000 kwamba taarifa hizo sio za kweli.
Zaha: The 21-year-old has found himself playing for the Under 21s this year instead of with the first team
'Sijawahi kuwa na mahusiano ya kmap3nzi wala kukutana na binti wa David Moyes, hivyo jambo hilo haliwezi kuwa sababu ya kukosa kwangu nafasi katika kikosi cha kwanza ...,' aliandika Zaha.
'Ningependa hizi taarifa za uongo ziachwe kusambazwa….Nitaichezea Manchester United pindi kocha atakapoana nipo tayari kufanya hivyo...'

Zaha aliichezea United katika mchezo wa kombe la hisani lakini tangu wakati huo ameichezea mechi moja tu ya mashindano dhidi ya Norwich City katika League Cup.


Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger