Angalia Picha zifuatazo zikikonesha washindi wa mashindano na wavumbuzi mbali mbali wa maajabu duniani wakipata jaza zao baada ya kutunukiwa na Guinness.
The Discovery Science Center in Santa Ana, California Kiliadhimisha kumbumbuku ya miaka 15 tangu kuundwa kwake kwa kutengeneza PUTO la ajabu ambalo ndani yake waliweza kuingia watu 118 ndani yake kwa ushirikiano kutoka kwa Fan Yang na Deni Yang wanafamilia ambao kwa miaka 27 wanajishughulisha na masula ya maputo na sabuni ambaopo watu hao 118waliingia na kutengeneza rekodi hiyo tare4, mwezi wa 4, 2011.
Mmarekani Ashrita Furman, a.k.a Mr. Versatility, ana zaidi ya rekodi 340 katika Guiness tangu mwaka 1979, kwa sasa anashikilia rekodi ya kukimbia kwa kasi zaidi kwa umbali wa maili moja ndani ya dakika 7 na sekunde 56 huku akiwa kavaa mavazi ya kuogelea na viatu vya kuogelea. Aliweka rekodi hiyo mwaka 2010 katika Marswiese Sportzentrum hukoVienna, Austria.
Ashrita Furman amewahi kuchukua rekodi katika nchi zaidi ya 35 katika mabara yote saba.
Mnamo mwaka 2008 Rekodi ya maajabu ya Guinness ilivunjwa tena ambapo zaidi ya watu 290000 katika nchi 15 tofauti walifanya mashibdano ya kukimbia kwa miguu na mikono yaani kama chura vile na.
Kenichi Ito wa Japan aliwafunika wote, kwani aliweza kukimbia umbali wa Mita 100 akiwa kama chura kwa kutumia sekunde 18.58 tu.
Amini Usiamini! Jama meweza kuwavuta watu wenye jumla ya uzito wa kilo 411.65 kwa kutumia kope za macho ambazo zilifungwa katika kamba na kufungwa kwenye ka baiskeli!
Rekodi hii ya aina yake iliandikwa na Chayne Hultgren, a.k.a "The Space Cowboy". Raia kutoka Australia aliandika rikodi hiyo huko Milano katika “Lo Show Dei Record” mnamo mwaka 2009. Mbali na hiyo, ameshawahi kushinda mashindano ya mtaani mara mbili mfululizo mnamo mwaka 2006 na 2007.
Mwezi Mei 2010, Chris Elliot na Tyson Turk (USA) waliweka rekodi ya watu waliojitoboa na kujivisha pete katika mwili wao kwa kuwa na pete 3100 ndani ya masaa 6 na dakika 15.Waliivunja rekodi iliyowekwa na muingereza Kam Ma na Charlie ya pete 1015 ndani ya saa 7 hours na dakika 55.