KUTOKANA na ndoa hiyo kuwa ya aina yake, hivi karibuni waandishi wetu walimuweka kati Bob Junior na kumbana kwa maswali ya “why, kwanini, ikawaje” aoe kimyakimya wakati yeye ndiye ‘prezidaa’ wa masharobaro?
Bob Junior akafunguka: “Nilifunga ndoa Desemba mwaka jana. Nililazimika kuoa kimyakimya kutokana na masharti ya wazazi wa pande zote mbili kwamba ndoa isifungwe kwa mbwembwe.”
Alisema, hata idadi ya wahudhuriaji katika ndoa hiyo ilidhibitiwa, hivyo kuruhusu ndugu na marafiki wachache kushuhudia tukio hilo.
“Kikubwa ni kufunga ndoa inayompendeza Mungu ili atupe Baraka zake na tuishi katika maisha yanayompendeza.
“Kwa Watanzania, napenda wajue tu ukweli kwamba nimeoa na mke wangu anatarajiwa kujifungua hivi karibuni,” alisema Bob Junior a.k.a Mr. Chocolate.
chanzo:.globalpublishers