Kakobe akana kulikacha Kanisa.


Askofu Kakobe aliyasema hayo, Januari 6, mwaka huu ndani ya kanisa lake alipokuwa akiwahutubia waumini wake na kusema ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari vilivyosambaza taarifa kuwa amelitoroka kanisa hilo, kitu ambacho si cha kweli. “Kunisingizia habari hizo ni kama wananiongezea maono sababu kweli natarajia kuondoka siku za hivi karibuni lakini sikusema ni lini na nitakwenda wapi,” alisema Kakobe. Akithibitisha juu ya uwepo wake katika kanisa hilo, kiongozi huyo aliendelea kufanya maombi na ibada zake kama kawaida huku mamia ya waumini wakisubiri uponyaji na wengine wakitoa ushuhuda juu ya miujiza waliyoipokea.


Chanzo. GPL.

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger