Wauza Miili yao na wateja wao wakamatwa Ndani ya Chumba Kimoja
Kwa tukio hili, vijana wa mjini wanasema; kimenuka! Hivi karibuni wanawake watano ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja walinaswa usiku mnene wakifanya mapenzi na wanaume wawili kwenye chumba kimoja kilichopo Mwananyamala jijini Dar.
Watu hao walinaswa katika oparesheni kabambe iliyoongozwa na Kamanda Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kinondoni, OCD Wilbroad Mtafungwa pamoja na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai.
Katika zoezi hilo, polisi walivamia kambi kuu inayotajwa kusheheni wanawake wanaojiuza iliyopo Mwananyamala A ambapo ‘wauza sukari’ hao hutumia vyumba vyao kufanya ufuska huo.
-->
Polisi hao walipofika kwenye chumba kimoja kilichopo eneo hilo, walikumbana na upinzani mkubwa wa watu waliokuwa ndani na baada ya kufanikiwa kuufungua mlango, waliwakuta wanawake watano na wanaume wawili wakiwa kimahaba.
Mbali na hao, polisi walifanikiwa kuwanasa wanawake wengine kwenye vyumba vyao na baadhi mtaani wakijiuza ambapo walipewa kibano cha hali ya juu.
Imeelezwa kuwa, wanawake hao wamekuwa na tabia ya kujiuza na wakati mwingine hukubali kufanya mapenzi na wanaume zaidi ya mmoja, hali ambayo ni hatari sana.
Mkazi mmoja wa eneo hilo, Husein Juma alisema: “Kwanza tunampongeza Kamanda Mtafungwa kwa operesheni hii, wanawake hawa wamekuwa ni tatizo kwani wamekuwa wakijiuza waziwazi na kutupa ovyo kondomu.
Naye Inspekta Swai alisema wamekuwa wakipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa eneo hilo wakaona ni vyema kuyafanyia kazi ambapo waliwakamata zaidi ya watu 35, wanawake kwa wanaume wanaohusika.