Mwanamke Ajinyonga Baada ya Kunyimwa Unyumba na Mumewe
Mwanamke mmoja Raia wa Zimbwambe amajinyonga na kamba baada ya kunyimwa mapenzi na mumewe kwa muda mrefu. Mama huyo afahamikaye kama Muhlava Muhlabiza kutoka kijiji cha Chigalo (64) alikutwa na umauti huo baada ya mumewe kurudi safarini na akijua ni zamu yake ya kupata haki hiyo ya tendo la ndoa ndipo mume huyo alipoghairi na kwenda kulala na mke mwingine, kitendo ambacho kiliumiza moyo wa mama huyo na kuamua kutokomea msituni na kujinyonga. --> Baada ya kupita kama saa moja mume wa mwanamke aliamua kutoka na kwenda kumgongea ndani kwake kwani alitishia kujiua na kusema ya kwamba mume huyo amemchoka na ndi[po alikuta kimya kimetawala na kuwataarifu watu ambao baada ya kuuvunja mlango hawakumkuta hadi kesho yeka walipata taarifa toka polisi kuhusu kupatikana kwa mwili wake msituni.