Mwandishi wa Habari Kikaangoni baada kutoa habari juu ya mabega ya Mhanga
Mwandishi mmoja wa habari huko India amejikuta katika wakati mgumu huku akitupiwa shutma na lawama kutoka makundi mbali mbali kwa kitendo chake cha kutoa taarifa ya mafuriko ambayo yameathiri watu zaidi ya 1000 na kuwaacha bila makazi huko India huku akiwa juu ya mabega ya mmoja ya waathirika hao. Katika utetezi wake mwandishi huyo amesema haikuwa dhamira yake na kwamba Mhanga huyo alijitolea mwenyewe kumbebe ikiwa ni sehemu ya kuonesha shukrani kutokana na msaada aliopewa na mwandishi huyo huku akitaka kuuonesha ulimwengu Madhara ya Mafuriko hayo hasahasa nyumbani kwake.