Hali ya Mandela bado si shwari
Hali ya Afya ya kiongozi wa Africa ya Kusini Mzee Nelson Mandela bado si shwari tangu alipolazwa tarehe nani mwezi huu akisumbuliwa na matatizo ya mapafu. Kutokana na kuzidi kudhohofika kwa afya ya Nguli na Mlezi wa Taifa hilo lenye maendeleo zaidi Kusini mwa Jangwa la Sahara, Imemlazimu Kiongozi wa Nchi hiyo Mzee Jacob Zuma Kuahirisha ziara yake ya nchini Msumbuji ambako alitakiwa kuwa msemaji katika kikao cha Masuala ya Miondombinu cha SADC Huko Maputo.Hali ya Afya Mzee Mandela mwenye umri wa miaka 94 imezidi kuwa mbaya ndani ya masaa 48 yaliyopita kiasi cha kuwaweka raia wa nchi hiyo tayari kwa lolote.