Baba Mzazi wa Kichanga Azuiwa kumwona mwanawe sababu ya kupata Ugonjwa wa ajabu wa Ngozi.
Baba Mzazi wa Mtoto mchanga Austin alikatazwa kuwa karibu au mumwona mtoto wake kwa kipindi kisichopunguz wiki mbili baada ya kukumbwa na ugonjwa wa ajabu wa ngozi.
Madakari walimshauri kutomsogelea mtoto huyo kwani baba mtu sehemu kubwa ya juu ya mwili hadi uso ulikuwa unaharibika siku hadi siku, kitendo kilichowapa hofu madaktari hao ya kwamba huenda Mtoto Austin angewea Kuathirika pia.
Tom Greenhalgh, 27 alianza kuonesha mabadiliko ya ajabu katika ngozi yake wiki mbili kabala mkewe, Kerry hajajifungua, alikuwa na tabia ya kujikuna sana ngozi yake na kila mara alikuwa akipata maumivu makali sana, Madaktari walihisi ugonjwa huo umesababaishwa na aina ya Moja ya Kirusi Kibaya cha magonjwa ya Ngozi.
Kwa zaidi ya siku mbili hali yake ilizidi kuwa mbaya mpaka alipoenda Hospitali ya Queens ambao walimpatia dawa za kupaka na Anti biotics pia walimshauri kumpumzika kazini maana alikuwa anahitajika kujitibu.
Tom na Familia yake baada ya kupona |