Kutolewa kwa Nando BBA,Furaha kwa Raia wa Ghana
Watu tofauti tofauti wamekuwa wakitoa maoni yao katika mitandao mbali mbali ya kijamii kuhusiana na Mtazamo wao juu ya kutolewa kwa Mshiriki kutoka Tanzania Nando katika jumba la BBA The Chase.
Nando alitolewa mara baada ya kikao cha dharula kilichomwita kumjulisha kuhusu makosa yake ambayo yalikuwa yanahatarisha mwenendo mzima wa BBA The Chase hasa baada ya kumpiga kibao mshiriki mwenzake, Elikem na kumtishia kumchoma kisu.
Furaha zaidi ni kwa mashabiki kutoka nchini Ghana ambao walipatwa na hasira baada ya Nando kumdhalilisha mshiriki kutoka nchi hiyo aliyeondolewa wiki 2 zilizopita.