Msanii JB Ala shavu


Na Denis Mtima
MWIGIZAJI Bora wa Kiume Bongo, Jacob Steven ‘JB’ amefuatwa na mastaa Wazungu kutoka Ulaya nchini Norway.
Hivi karibuni, Ijumaa Wikienda lilimnasa JB akipigwa na baridi usiku wa manane kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar ambapo alipoulizwa kulikoni alisema kuna waigizaji kutoka Norway wanaokuja kumfuata hivyo anawasubiri.
Alisema: “Kuna waigizaji Wazungu kutoka Norway wanakuja kunifuata, nimekuwa nikiwasiliana nao kwa muda mrefu, mwanzoni nilisita kwa kuwa nilikuwa siwajui. Baadaye nilijiwa na mawazo kwamba kwa nini nisiwatafute mtandaoni? Kweli nilipoingia mtandaoni na kutafuta majina yao niliwapata.
“Wapo wawili, majina yao ni Bard Yuvis Akir na Vega Uvisakir, waliniambia wanakuja kunichukua nikafanye nao kazi za filamu kwao, nikimaliza Tamasha la Matumaini tutarekodi filamu moja hapa nchini ndiyo tuondoke.”
wakati mazungumzo yakiendelea, JB aliitwa kwenye mlango wa kutokea uwanja wa ndege na kuwapokea wageni wake kisha kutimua eneo hilo.

Source:- Global Publishers

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger