Obama Atua Dar, Kukutana Na Bush Kesho
Rais wa Marekani, Barrack Obama amewasili jijini Dar Es Salaam leo majira ya saa nane mchana na kupokelewa na mamia ya wananchi pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali huku kukiwa na ulinzi mkali kutoka vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania na Marekani. Katika ziara yake hiyo yenye lengo la kuongeza na kukuza ushirikiano wa kibiashara baina ya Nchi zinazoendelea na mataifa yaliyoendelea.
Rais Obama anatarajia kutembelea kiwanda cha uzalishaji umeme cha Symbion cha Wamerekani, ziara hiyo imekuja miezi mitatu baada ya ziara ya Raisi wa China, ikionesha ni jinsi gani mataifa haya yamo katika ushindani wa kibiashara na rasilimali kutoka katika nchi zinazoendelea, hususani Tanzania. Rais Obama pia anatarajia kukutana na Rais Mstaafu George Bush ambaye yupo Nchini kwa ajili ya Taasisi yake na pia wawili hao wanatarijia kuonana kwa ajili ya kuweka mashada ya kumbukumbu ya watu waliofariki kutokana na milipuko ya mabomu katika ubalozi wa marekani mwaka 1998.