Wabunge wa Nigeria wataona damu sababu ya kupishana kisiasa, angalia picha wakizichapa Bungeni.


Juzi kumeibuka ugomvi wa Aina yake katika Bunge la Nigeria kiasi cha kusababisha wabunge zaidi ya watano kujeruhiwa. Ugomvi huo uliotokana na upinzani wa kisiasa juu ya mswaada ulioanza kujadiliwa miezi miwili iliyopita.

Imeelezwa ya kwamba mmoja wa wabunge hao aliwaandaa vijana wake wa kazi kwa ajili ya kuleta uchavuzi huo na ya kwamba walitangulia kufika eneo la tukio mapema hata kabla ya kikao kuanza.

Mara baada ya hali ya hewa kuchafuka mjengoni hapo, wabunge hao walianza kubeba mitungi ya vioo na vyuma vya mapambo na kuanza kupigina hali iliyosababisha wengi wao kujeruhiwa akiwemo spika wa Bunge Hilo.

Baadhi ya wabunge walitimua mbio ili kujinusuru na majeruhi wengi wamepelekwa katika kituo cha afya cha St Patricks Hospital  maeneo ya Ogbunabali katika Port Harcourt 


Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger