Ahadi za Mwanaume wake ni 'Kitandani tu" akimaliza anasahau kila kitu.
Habari hii nimeikuta sehemu, nami nimeileta huku, Analalamika Mwanada huyu ambaye yuko katika mahusiano ya Kimapenz na Mwanaume wake kwa zaidi ya mwaka sasa, kinachompa wakati mgumu ni tabia ya mpenz wake huyo kutoa ahadi kibao hasa za kumuoa pindi wanapokuwa "Faragha" lakini akishamaliza haja zake jamaa anasahau ahadi zote.
Kwa upande wake, mwanamke anashindwa la kufanya huku akiwa anaona aibu na kuhofia itakuwaje mwanaume huyo akikasirika na kumuacha, hivyo anaomba ushauri nini afanye.