Chris Brown matatani kwa shambulizi kwenye hoteli ya nyota tano mjini Washington DC
Na MOblog Team kwa msaada wa mtandao
Mwanamuziki maarufu nchini Marekani Chris Brown yu matatani tena kwa kufanya shambulizi la mwilini kwa kumpiga ngumi na kumsukuma mmoja wa wageni katika moja ya Hoteli ya hadhi ya nyota tano jijini Washington, DC majira ya asubuhi ya 4.30 na kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwenye moja ya kituo cha Polisi jijini huo.
Tukio hilo limefanyika jijini Washington, DC na limesababisha mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kukamatwa kwa shambulio hilo.
kwa mujibu wa sheria za Marekani, mtu akifanya kosa la kumshambulia mwenzake anaweza kwenda jela kwa miaka minne, Brown gwiji la muziki wa R’n'B ambaye alipewa kifungo cha nje kama msamaha kwa kosa kama hilo kwa kumshambulia mpenzi wake wa zamani Rihanna mwaka 2009.
Gari za Polisi likiwa limezingira basi la Chris Brown (Tour Bus) analotumia kwenye safari zake za muziki likiwa nje ya Hoteli aliyolala jijini Washington DC.
Brown na walinzi wake wote wamekamatwa kwa mahojiano zaidi baada ya mwanamuziki huyo kumshambulia mmoja wa wageni katika hoteli hiyo ya nyota tano jijini Washington D.C.
kwa kawaida Chris na mpenzi wake Rihanna huwa wana tabia ya kugombana baada ya matumizi ya madawa ya kulevya lakini siku hiyo Rihanna hakuwa katika ushawishi wa madawa ya kulevya au pombe.
Mabishano yalitokea katika kulizunguka gari la Brown baada ya walinzi wake kutaka kugomea amri ya polisi ya kumkamata mapema jioni ya siku ya tukio lakini baadaye alipelekwa kituo cha polisi chini ya ulinzi mkali. Mwathirika wa tukio hilo alivunjika pua na kupelekwa hospitali kwa matibabu.
Chanzo cha habari kinasema sababu hasa ya Brown kumpiga mtu huyo akijajulikana mara moja
Kengete Blog.