"Sipo tayari kumvulia nguo bwana Misosi, labda anibake." Amanda
Staa wa sinema za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa hawezi kurudia makosa tena kwa kumvulia nguo aliyekuwa mpenzi wake, Joseph Rashau ‘Bwana Misosi’.
Akiongea na mwandishi wetu muda mchache baada ya wadau kibao kumtaka mwanadada huyo arudiane na mpenzi wake huyo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, Amanda alisema tayari ameshapenda kwingine hivyo hapendi kumzungumzia mtu aliyeachana naye pia hana tabia ya kurudia matapishi yake.
"Sipo tayari kumvulia nguo bwana Misosi, labda anibake, kwani nikishaachana na mtu huwa namtoa moyoni kabisa na ndio maana sipendi hata kusikia lolote juu yake"..Alisema Amanda