AMUUA MKEWE NA MIMBA YA MIEZI TISA TUMBONI
JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, linamshikilia Philemon Ng’ambi, mkazi wa Madale Kata ya Wazo, jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kumuua mkewe, Enea Kagine kwa kumshambulia kwa mawe na matofali hadi kumuua.
Philemon anadaiwa kufanya unyama huo kwa marehemu mkewe aliyekuwa amebakiza siku mbili kabla ya kujivungua usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita nyumbani kwake Wazo-Hill.
Akisimulia mkasa huo kwa mapaparazi wetu, jirani wa wanandoa hao aliyejitambulisha kwa jina la Fikiri Rashid alisema:
“Mimi nyumba yangu na yao zinatazamana hivyo siku ya tukio majira ya saa tisa usiku, nilianza kumsikia marehemu akipiga mayowe ya kuomba msaada akisema mumewe anamuua.
“Mimi nyumba yangu na yao zinatazamana hivyo siku ya tukio majira ya saa tisa usiku, nilianza kumsikia marehemu akipiga mayowe ya kuomba msaada akisema mumewe anamuua.
“Nilitoka nje kwa lengo la kutaka kutoa msaada lakini nilihofia maisha yangu hivyo ilinibidi niwaite vijana wa ulinzi shirikishi ambao baada ya muda walifika eneo la tukio na kumkuta mtuhumiwa akivunja vyombo vya ndani kama mtu aliyechanganyikiwa, wakati huo tayari alikuwa ameshamuua mkewe.
“Baada ya kuwaona ulinzi shirikishi, alikimbilia chumbani na kwenda kujificha uvunguni kwenye kitanda huku watoto wao watatu wakiwa wamelala.
“Bila kuchelewa, askari wa ulinzi shirikishi walimkamata na kuwasiliana na Askari wa Kituo cha Polisi cha Wazo ambao walifika eneo la tukio na kumtia mbaroni mtuhumiwa pamoja na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya taratibu za kipolisi,” alisema Fikiri.
Kufuatia tukio hilo la kusikitisha wanahabari wetu walifika katika Hospitali ya Mwananyamala ulipohifadhiwa mwili wa mwanamke huyo na mtoto wake waliyemtoa akiwa amefia tumboni.
Miili hiyo ilizikwa Jumatatu iliyopita (Novemba 25) mwaka huu katika kaburi moja kwenye Makaburi ya Madale, Dar es Salaam.
GPL