HABARI MBAYA KWA WAISLAMU NCHINI, ANGOLA WAPIGA MARUFUKU UISLAMU KWAO.
Serikali ya nchi ya Angola imeamuru kufungwa kwa Misikiti yote kisha kuziondoa na sheria za Kiislam nchini humo.
“Kuruhusiwa kwa Uislam ni kitu ambacho hakijapitishwa na Wizara ya Sheria na Haki za Binadamu na ni kwamba Misikiti yao itafungwa mpaka taarifa itakapotolewa,” alisema Waziri wa Utamaduni wa nchi hiyo Rosa Cruz e Silva.
Waziri huyo ameuelezea Uislamu kama ni sehemu ambayo inabidi iondolewe sababu unapingana na mila na desturi za Angola.
Kufuatia hatua hiyo ya Angola kumekuwa na taarifa zisizo rasmi kwamba Misikiti mingi iliyopo Kusini mwa Afrika imekuwa ikiondolewa.
“Huu ni mwisho wa Uislamu ndani ya nchi yetu,” Rais Jose Edurado dos Santos aliieleza gazeti la Osun Defence.
Waislamu nchini Angola wapo chini ya 1% ya idadi ya watu millioni 19 wa nchi hiyo, huku zaidi ya nusu ya watu wa nchi hiyo ambayo ilitawaliwa na Ureno kuwa ni Wakristu.
Dan Chibo.