Housegeli abakwa na kulawitiwa na bosi wake huko Arusha
VITENDO vya ukatili kwa watoto wenye umri mdogo vimeendelea kushamiri katika jamii, ambapo msichana wa kazi aliyetambulika kwa jina la Anna (13) mkazi wa ngaramtoni wilayani arumeru mkoaani arusha, ameharibika vibaya sehemu zake za siri kutokana na kitendo cha kunajisiwa na kulawitiwa na baba mwenye nyumba wake aliyejulikana kwa jina la Godifrey John(33).
Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kuokolewa na shirika la shaloom center for street children, linalojihusisha na utetezi wa haki za mtoto, mtoto huyo anaeleza kuwa, alianza kufanyiwa vitendo vya ukatili tangu April mwaka huu baada ya kutoka kijijini kwao masumbwe kilichopo wilayani kahama, mkoa wa shinyanga.
Alisema kitendo hicho kilikuwa kikimuumiza sana, lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga alilazimika kuzoea maumivu makali aliyokuwa akiyapata kwani mwajiri wake alikuwa akishamaliza kumwingilia alikuwa akimtishia kumuua iwapo angethubutu kutoboa siri hiyo kwa mtu yeyote.
Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano, anaeleza kuwa, bosi wake huyo ambaye pia ni mfanyabiashara wa mazao, alikuwa akimnajisi na kumlawiti kwa kumziba mdomo ili asitoe sauti baada ya kumfungia mke wake chumbani majira ya usiku na mchana hasa kipindi ambacho mkewe alikuwa kwenye hali ya kujifungua.
Alisema bosi wake huyo alikuwa akimwacha mkewe kitandani na kumfuata sebuleni alikokuwa amelala na kuanza kumwingilia kinyume na maumbile huku akiwa amemziba mdomo ili asitoe kelele wakati akifanyiwa ukatili huo.
''Alikuwa akiniingilia mara kwa mara, sikumbuki ni mara ngapi, na akianza kunifanyia mchezo mbaya alikuwa akiniziba mdomo na mkewe alikuwa akimfungia chumbani kwa komeo na kuna kipindi alikuwa mkali akinikaripia'' alisema.
Alisema kuwa, alifika mkoani arusha, mwezi februari mwaka huu, baada ya kuchukuliwa na mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la zawadi samuel ambaye ni rafiki yake na mtuhumiwa, ambaye alikuwa akihitaji msichana wa kazi kutokana na mkewe kuwa mjamzito.
"Huyo zawadi tulikutana nae kwenye basi nikitoka masumbwe kwenda kahama mjini, akaniambia kuwa anipeleke arusha akanitafutie kazi, nilikubali tukaondoka kesho yake, ila hadi sasa sina mawasiliano na wazazi wangu na sina ndugu yeyote hapa arusha,'' alisema anna.
Aliongeza kuwa katika kipindi cha miezi 8 alichofanya kazi kwa mtuhumiwa huyo, hakuwahi kulipwa mshahara ambao walikubaliana shilingi 20,000 kwa mwezi, ila aliwahi kumpa shilingi 10,000 na kumnunulia sketi mbili tu.
Alieleza kuwa mbali na kumfanyia unyama, alikuwa akimtesa kwa kumfanyisha kazi nyingi ikiwemo kumlazimisha kusomba maji umbali mrefu bila kupumzika, huku akishindwa kumsomesha kama alivyoahidi kufanya hivyo hapo awali.
Kwa upande wa mwakilishi wa shirika la shaloom center, Enezael Joseph alisema kuwa wamefanikiwa kumwokoa mtoto huyo katika mazingira magumu baada ya kupata taarifa kuwa amekuwa akifanyiwa vitendo vya unyanyasaji kinyume cha sheria.
Alisema kuwa shirika hilo lilipata taarifa kutoka kwa majirani wa mtuhumiwa ambao walichoshwa na vitendo vya manyanyaso anavyovipata mtoto huyo na kuamua kumfuata mtoto huyo na kuzungumza naye ndipo alieleza mambo mazito ya kulawitiwa na kunajisiwa naa mtuhumiwa kila kukicha.
Joseph anasema kuwa baada ya taarifa hizo walitoa taarifa kituo cha polisi ngaramtoni na kupewa hati ya matibabu (PF3) ambapo msichana huyo baada ya kupimwa katika hospitali ya seliani ya jijini arusha, aligundulika kuharibiwa vibaya sehemu zake zote za siri.
Alisema baada ya kupata majibu ya dakitari walirejea na kuwakabidhi polisi ambapo walifungua hati ya mashtaka ya kulawiti yenye kumbukumbu namba NGT/RB/1113/2013 ambapo mtuhumiwa alikamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaaendelea.
Hata hivyo mtuhumiwa wakati akitiwa mbaroni alisikika akidai kwamba anachofahamu kwa msichana huyo ni kwamba anamdai fedha zake za mshahara ila hayo madai mengine si kweli kwani amepandikizwa ili kumdhalilisha.