Jack wa Maisha Plus naye atumbukia katika Tabia Chafu
MREMBO aliyeshiriki Shindano la Maisha Plus Season 2, Jacqueline Dunstan ‘Jack wa Maisha Plus’ amezua jambo katika mtandao baada ya kutundika picha akiwa anabusiana na mwanamke mwenzake.
Jack ambaye kwa sasa yupo nchini Dubai, aliweka picha hiyo katika mtandao wa Instagram hali ambayo iliwashangaza wadau wengi waliopo kwenye mtandao huo ambapo walimchana kuwa aache vitendo vya kisagaji lakini mwenyewe hakujibu.
Jack baada ya kuweka picha hiyo aliandika maneno haya; ‘mwaaah’ ndipo wadau walipoanza kumshambulia na kumtaka aondoe picha hiyo chafu.
GPL