Magaidi Waitikisa Tena Kenya, wawili wauawa katika shambulizi la Jana


Taarifa ya  kituo cha TV cha KTN Kenya inasema washukiwa wawili wa Ugaidi kwenye mtaa wa Eastleigh wakidaiwa kuwa miongoni mwa genge lililoshambulia msikiti kwenye mtaa huo December 2012 na kumjeruhi Mbunge wa Kamkunji Yusuf Hassan, wameuwawa asubuhi ya November 13 2013.

Mtaa huo ambao unaaminika kuwa chimbuko la Wanamgambo wa kundi la kigaidi la Al Shabaab ambapo mwaka huo wa 2012 washukiwa hao walifanikiwa kutoroka, mmoja kwa gari na mwingine kwa miguu umeshuhudia washukiwa hao wakiuwawa na Polisi waliokua wakiwasaka kwa muda kabla ya kuwapata.

Walioshuhudia kisa hiki kipya wanasema Polisi walitaka wajisalimishe lakini wakagoma hivyo wakaamua kuwaua kwa risasi kwenye mtaa huu huu wenye Wakimbizi laki sita kutoka Somalia ambao hawajasajiliwa huku hiyo ikisemekana kuwa njia rahisi kwa Wanamgambo wa Al Shabaab kuingia Kenya.



Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger