Mtoto anaishangaza Dunia kwa Ulevi wa Kula na Kuvuta Sigara kupita kiasi.
Akiwa na umri wa miaka miwili tu, mtoto huyu wa ajabu ameishangaza Dunia mara baada ya picha na habari zake kusambaa zikieleza na kumuonyesha akiwa anavuta sigara kupitiliza.
Sasa, akiwa na umri wa miaka 5, inaelezwa kuwa ameachana na tabia hiyo, ila kwa sasa ameanzisha tabia mpya ya kula kwa kupitiliza..
Mtoto huyu anaitwa Aldi Rizal alikutwa kijiji kimoja cha watu wa maisha ya chini kiitwacho Sumatra, nchini Indonesia, akiwa anavuta sigara mfululizo bila kuacha.