Taswira katika ajali iliyoua watu 7 huko Morogoro Leo


...Wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya ajali hiyo.…

Toyota Noah yenye namba za usajili T502 AUP iliyokuwa ikitoka wilaya ya Gairo kuelekea Morogoro mjini baada ya kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania lenye namba za usajili T129 AGB.
...Wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya ajali hiyo.
...Muonekano wa Toyota Noah kwa nyuma baada ya ajali.
...Ndani ya Toyota Noah baada ya ajali.
Lori aina ya Scania lenye namba za usajili T129 AGB ambalo lilikuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Tabora baada ya kugongana uso kwa uso na Toyota Noah yenye namba za usajili T502 AUP.
Lori aina ya Scania lenye namba za usajili T129 AGB baada ya ajali.
 
WATU saba wamekufa papo hapo kwenye ajali mbaya iliyotoka leo alfajiri katika kijiji cha Dakawa - Sokoine Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro. Ajali hiyo iliyohusisha gari ya abiria aina ya Noah yenye namba za usajili T 502 AUP iliyokuwa ikitoka Wilaya ya Gairo kuelekea Morogoro mjini kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania lenye namba za usajili T129 AGB ambalo lilikuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Tabora.

Watu saba wamepoteza maisha katika ajali huyo akiwemo dereva wa Noah aliyejulikana kwa jina la Masoud Juma na wengine wanne hali zao ni mbaya.

 "Chanzo cha ajali hii ni dereva wa Noah ambaye alikuwa akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake na ghafla akakutana na lori uso kwa uso" Alisema Bw. Sanjo Ole ambaye ni mfugaji jamii ya Kimasai.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile amedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
 
CREDIT: globalpublishers.info



Read more: http://mambomseto88.blogspot.com/2013/11/updates-taswira-ya-mapicha-katika-ajali.html#ixzz2l1rPhS3i

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger