Hoteli Hii Inauza Nyama za Binadamu, Wananchi watahadharishwa Kuwa Makini
Polisi wapatao 11 walivamia Hoteli hiyo (Jina Limehifadhiwa) ambayo ipo karibu na soko la Okwodu Huku Anambra na kukuta vichwa viwili vya binadamu vikionesha kuuawa muda si mrefu.
Polisi hao walipewa taarifa na Wasamaria wema kuhusu kuwa na mashaka na mwenendo wa Hoteli hiyo na ndipo Jeshi la Polisi lilipofanya uvamizi huo na kujionea mambo hayo, Pia Polisi waliweza Bunduki Mbili, Kofia Mbili za Jeshi na Mizunguko 40 ya Risasi pamoja na simu kibao za Mkononi.
" Kila nikiwa nakuja Sokoni nimekuwa nikijionea hali isiyokuwa ya kawaida na mizunguko ya ajabu karibu na Hoteli hiyo, kuna kipindi huwa nawaona watu wa hatari hatari ambao huwa wanatia wasiwasi wakiingia na kutoka hotelini hapo, hivyo sijashtuka kuoona wamevamiwa na polisi asubuhi ya Jana" Alisema Muuza Mboga Katika Eneo Hilo.
Pia Mchungaji mmoja aliwahi kuwadokeza Polisi kuhusu Kulipishwa Bei isiyokuwa ya kawaida baada ya kula nyama Hotelini hapo. Hakujua ya kwamba ni nyama ya Binadamu.