Ryan Gigs atimiza Miaka 40 leo, bado yupo yupo kwanza na Man U.


Kiungo wa klabu ya Manchester United Ryan Giggs hana mpango wa kustaafu japokuwa leo Ijumaa akiwa anatimiza miaka 40.

Mchezaji huyo toka Wales ametumia muda wake wote wa mpira akiwa anachezea timu hiyo toka Old Trafford, akiicheza klabu hiyo jumla ya mechi 953 tok alipoanza kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Everton mnamo mwaka 1991.

"Nina bahati kwamba nimekuwa kwenye klabu moja. ambapo nimezungukwa na wachzaji wazuri na meneja mzuri," alisema.

"Inaweza kuwa ngumu wakati mwengine ila bado nafurahia, vyovyote itakavyokuwa nitaendelea."

Akaongeza: "Nahitaji kufanya vyema kwenye kila mchezo, nataka kushinda mataji na lengo langu nikuwa kwenye hilo."


Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger