TASWIRA MSIBANI KWA MWANAUME ALIYESABABISHA MAUAJI ILALA NA KISHA KUJIUA MWENYEWE
Ni Gabriel Munissi ambae alijiua kwa risasi Ilala Dar es salaam November 19 2013 baada ya kuua watu wengine wawili kwa risasi asubuhi kati ya saa moja na saa mbili, amezikwa kwao Nkoshashi Wilaya ya Hai Kilimanjaro leo November 22 2013.
Gabriel ambae amefariki akiwa na umri wa miaka 31, anadaiwa kufanya mauaji ya watu wawili aliowasubiria nje ya geiti wakitoka nyumbani kwao (waliouwawa) huku chanzo kikitajwa kwamba ni kisa cha kimapenzi.
Kama alijua kitakachotokea, alichokiandika cha mwisho kwenye page yake ya facebook kiko chini kabisa mwa hii post.