Watu 50 wafariki katika ajali ya ndege Urusi leo.
Imeripotiwa kuwa Ndege Aina ya Boeing 737 iliyokuwa inataka kutua katika uwanja wa ndege wa Kazan ikitokea Mjini Moscow huko Urusi imedondoka na kulipuka moto na kuua watu wote 50 waliokuwa ndani ya ndege hiyo.
Katika idadi hiyo jumla ya abiria ilikuwa ni 44 na wafanyakazi 6. Ingawa Urusi ni Nchi iliyoendelea lakini ina kabiliwa na rekodi mbaya ya ajali za ndege hasa ndege za abiria wachache. Vyombo vya usalama bado vinachunguza kujua nini hasa kimesababisha ajali hiyo.
Magari ya kubebea wagonjwa yalionekana eneo la Uwanja wa Ndege jijini Kazn, Urusi.