CECAFA Challenge:MBWANA SAMATA NA THOMAS ULIMWENGU WAIPELEKA STARZ ROBO FAINALI


TIMU ya Taifa ya Tanzania bara, The Kilimanjaro Stars imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika mashariki na kati, CECAFA baada ya kuitafuna Burundi bao 1-0 alasiri ya leo.

Shukurani kubwa zimwendee nyota wa Tanzania anayekipiga klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samatta aliyefunga bao hilo pekee katika dakika ya 7 akiunganisha kwa ufundi mkubwa krosi iliyochongwa na Mtanzania mwenzake anayekipiga klabu ya Tp Mazembe, Thomas Ulimwengu.

Stars imecheza soka zuri na kupata nafasi nyingi za kufunga, lakini umahiri wa kipa wa Burundi, Arakaze Arthur amewaokoa Warundi kwani aliokoa bunduki nyingi langoni mwake.
Kwa Matokeo ya mchezo wa leo, Kili Stars imemaliza mechi za makundi ikijikusanyia pointi 7 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Zambia, kisha kuifunga Somalia 1-0 mechi za awali, na leo hii kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burundi.

Nani atakuwa kinara wa kundi B, matokeo ya mchezo unaoendelea sasa baina ya Zambia na Somalia utaamua ambapo mpaka sasa ni mapumziko na Zambia wako mbele kwa mabao 2-0.
Kama Zambia itaibuka na ushindi mkubwa leo hii basi itaongoza kundi B, na tafsiri yake ni kuwa Kilimanjaro Stars itakumbana na Uganda katika mchezo wa robo fainali.

Iwapo Kili stars itakutana na Uganda, itakuwa na hamu ya kulipa kisasi kwani walilala 3-0 katika mchezo wa nusu fainali wa michuano iliyopita mjini Kampala, Khamis Kiiza na Emmanuel Okwi wakiwemo ndani kwani mwaka huu pia wamejumuishwa kwenye kikosi cha Uganda The Cranes.
kama Stars itaongoza Kundi B, itakutana na Timu ya Taifa ya Rwanda, `Amavubi` .
Tanzania Bara;

Ivo Mapunda, Himid Mao, Erasto Nyoni, Said Morad, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Amri Kiemba/Haroun Chanongo dk77, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Mrisho Ngassa/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk81.

Burundi;
Arakaza Arthur, Hakizimana Hassan/Abdulrazack Fiston dk81, Hererimana Rashid, Hakizimana Issa, Nsabiyumva Frederic, Nduwimana Jean, Ndikumana Yussuf, Duhayinavyi Gael/Mussa Mosi, Nduwarugira Christophe, Habonimana Celestin na Hussein Shaaban/Ndarusanze Claude.

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger