GRACA MACHEL, MJANE WA MANDELA NA SAMORA MACHEL



ANAITWA Graca Simbine Machel ni Mmozambique (Msumbiji). Kufuatia kifo cha rais wa kwanza wa Afrika Kusini huru, Nelson Mandela (95) kilichotokea usiku wa kuamkia jana, Graca anakuwa mwanamke pekee duniani kuwa mjane wa marais wawili kwenye nchi mbili tofauti.
Marehemu Nelson Mandela (kushoto) na Graca Machel.
Mwaka 1975 hadi 1986, Graca alikuwa mke wa Rais wa Msumbiji, marehemu Samora Moses  Machel.  Wakati huo, Graca alikuwa waziri wa elimu na utamaduni wa nchi hiyo.
Baada ya kifo cha mumewe kilichotokea kwa ajali ya ndege mwaka 1986, Graca aliishi mjane hadi mwaka 1998 ambapo alifunga ndoa na Nelson Mandela akiwa rais wa kwanza wa Afrika Kusini huru.  Ni baada ya Mandela kumtaliki mkewe wa pili, Winnie Madikizele Mandela kwa madai ya kutokuwa mwaminifu katika ndoa.



Kuanzia hapo mwanamama huyo alianza kutambulika kwa jina la Graca Machel Mandela.
Hata hivyo, Graca alishika nafasi ya u-first lady wa ‘Sauz’ kwa mwaka mmoja tu, 1999 mumewe hakugombea tena urais.
Kifo cha mumewe kimempa ujane mwingine unaodaiwa kutotokea duniani, kuolewa na rais, rais kufa, kuolewa na rais mwingine naye kufa.

HISTORIA YA GRACA KWA UFUPI
Graca alizaliwa Oktoba 17, 1945 katika Jimbo la  Gaza nchini Msumbiji.
Alipata elimu ya msingi jimboni humo, elimu yake ya chuo kikuu aliipatia Lisbon, Ureno.
Ana watoto wawili, Malengani na Josina  aliowapata kwa marehemu Machel. Hakupata mtoto kwa Mandela.

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger