Baba ampiga mwanaye hadi kifo kwa sababu ya Udokozi.

-->
Raia mmoja mwenye hasira amemua mwanye baada ya kumshishia kipigo kikali kwa kosa la jaribio la kuiba katika nyumba ya jirani. Orugundage Ahmed, 34 amemua mwanaye Qudus usiku wa tarehe 27/06/2013 mbele ya mtoto wake wa kike Sherifat, na kisha kumchia shimo/kaburi uani na kumzika.

Baadhi ya majirani wanaoishi karibu na mwanaume huyo wamesema kwamba walisikia sauti ya kupigwa na kelele za kijana huyo lakini walishindwa kuingilia maana baba yake ni mkorofi na hawakupenda usumbufu wake. Imeelezwa kuwa kuna muda mzee huyo humpiga mwanawe mfulilizo kuanzia saa 11 jioni hadi saa moja usiku.

Siku ya tukio baada ya kijana huyo kukamatwa kwa jirani na kukabidhiwa kwa baba yake, Orugundage alianza kumpiga na waya mgumu kwa zaidi ya masaa matatu mfulilizo. Majiani walisikia kelele za kijana huyo lakini walikaa majumbani kwao.

Ilipofika saa moja na nusu usiku walimwona mzee huyo akitoka uwani na kuanza kuchimba shimo, hapo wakahisi kuna tukio limekuta kijana huyo na ndipo walipoaamua kupiga simu polisi, lakini polisi hawakufika mpaka kiongozi wa kimila wa eneo hilo alipopata taarifa na ndipo polisi walikuja kumkamata baba huyo.

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger