Hatimaye "MATONYA" wa England Warudishwa Kwao Romania

Safari Imeiva baada ya kuvamiwa Alfajiri

Makazi yao hata kwa Mtogole kuna nafuu

Waliokubali kuondoka, na mifuko ya Ki Nigeria kama uswazini kwetu
Lile kundi la watu zaidi ya 62 ambalo limekuwa kero kwa zaidi ya wiki kadhaa katika mitaa ya Hyde park Karibu na Hotel kubwa ya Kifahari ya Dorchester Hotel huko Uingereza. Raia hao kutoka Romania waliweza kujenga makazi yao duni katika eneo moja la wazi kitendo ambacho kilikuwa kinawakera wenyeji wa hapo kwani licha ya kuwa wanachafua mazingira, wageni hao walikuwa na kawaida ya kuomba omba misaada toka kwa wakazi na wapita njia.

Asubuhi ya Leo kundi la Askari Polisi walifika katika eneo hilo na kuwaeleza ya kwamba kwa hiari yao waondoke kwao na ndege ipo ya bure au wanaotaka kubaki basi wataenda jela. Katika Umati huo wote, ni watano tu waliokuwa na kibali ya kuishi na kufanya kazi nchini humo.

Haya sasa" Nani Kasema Ulaya Hakuna Omba Omba?"



Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger