Maajabu!!! Mbuzi azaliwa akiwa na "Vichwa" Viwili!!
Kuanzia Saa 10 Alfajiri zilisikika kelele za Maumivu kutoka kwa mbuzi jike ambaye alikuwa anajifungua, Kelele zilikuwa kubwa mno kuashiria maumivu makali alikuwa anayapata kiumbe huyo, palipozidi kupambazuka ilibidi majirani waende kushuhudia kulikoni kwa mbuzi kuwa na kelele kiasi kile, na ndipo walipojionea maajabu baada ya mbuzi jike huyo kujifungua watoto watatu, wawili kati ya hao wakiwa ni wa kawaida kabisa na mmoja akiwa na vichwa viwili.
Hayo ndio yaliyojiri Alhamisi ya jana tarehe 18 July 2013 Huku katika Jimbo la Irolini Kwara, Nigeria. Hata hivyo mbuzi huyo alizaliwa na vichwa viwili alifariki saa chache baadae.