Sexy Pokello na Bassey Watolewa katika Jumba la BBA The Chase.


Pokello

Safari ya Kufunga Virago kwa washiriki wa BBA The Chase Kutoka Nchini Zimbabwe (Pokello) na Sierra Leone (Bassey) Imeiva. Wawili hao wametolewa baada ya kupata kura chache za kuwafanya wabaki ndani ya jumba hilo.

Pokello alishaingiz katika kinyang'anyiro cha kutolewa kwa zaidi ya mara nne na mara zote alikuwa akipata msaada toka nchi za Nigeria na Ghana ambao alikuwa akiwasihi wambebe.

Safari hii bahati ya mshiriki huyo imekataa baada ya kuwasema vibaya waokoaji hao hasa wa Nigeria kwamba waandaaji wa shindano hilo huwa na tabia ya kuwapendelea hao Wa Nigeria ili wapate ushindi huku akitolea mfano tukio la mwaka 2010 ambapo mshiriki kutoka Nigeria, Uti alipendelewa na mshiriki kutoka Zimbwabwe, Munya alifanyiwa fitina.

Kwa kauli yake hiyo, ameponzeka. Wengi wamesikitishwa kwa kutolewa kwa mshiriki kutoka Sierra Lionne, huku wakisema kwa Pokello ni sawa sawa kwani walishachoshwa na vijimambo vyake.


Bassey kutoka Sierra Lionne


Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger