"Niite Tena Boss Mfupi Uone Ntakufanya Nini" Aki
Muigizaji Kutoka Nchini Nigeria, Chinedu Ikedieze, maarufu kama Aki, amewatahadharisha mashabiki wake wanaomfuata kupitia twitter kamwe wasimuite "BOSS MFUPI" kwasababu anachukizwa na jina hilo, na badala yake wamuite The Boss tu au vinginevyo atawa block wasiwasiweze kuwasiliana tena.
Aki ambaye aliwika sana kipindi cha Movies za " Aki na Ukwa", si mtoto tena, kwani ameshaoa Tangu mwaka 2011, na Mwanamke Huyo Hapo Juu katika picha.