Azam Wamlamba Mnyama 2-1, Wakaa kileleni mwa Ligi.
Timu ya Soka ya Azam FC Jana imefanikiwa kuiondoa Simba katika usukani wa Ligi Kuu soka Tanzania bara baada ya kuichapa goli 2-1 katika mchezo wa 11 wa timu hizo kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara. magoli ya Azam yalifungwa na Kipre Chetche huku la Simba likifungwa na Ramadhan Singano 'Messi'.
COASTAL Union ya Tanga imezinduka baada ya sare na vipigo vilivyofuatana,nayo ikiifunga Mtibwa Sugar ya Morogoro mabao 3-0 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Coastal ambayo sasa iko chini ya makocha wa muda, wachezaji wake wa zamani, beki Joseph Lazaro na mshambuliaji Razack Yussuf ‘Careca’ ilipata mabao yake leo kupitia kwa viungo Wakenya Crispin Odula dakika ya 20, Jerry Santo 38 kwa penalti na mshambuliaji mzawa, Danny Lyanga dakika ya 88.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, Ruvu Shooting imetoka sare ya 1-1 na Kagera Sugar ya Bukoba, Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani. Kagera Sugar ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mpachika mabao wake mahiri, Themi Felix dakika ya 36 na Said Dilunga akaisawazishia Ruvu dakika ya 72. Kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, wenyeji JKT Oljoro wamelazimishwa sare ya bila kufungana wa ‘Watoto wa Jiji’, Ashanti United ya Ilala, Dar es Salaam. |
---|
MSIMAMO WALIGI
|
---|