Jamal Malinzi ashinda urais wa TFF


Habari tulizozipata  ni kwamba Jamal  emil Malinzi amefanikiwa kushinda uchaguzi wa TFF kwa nafasi ya urais aliyokuwa anagombea dhidi ya Makamu wa zamani wa Rais wa TFF Athumani Nyamlani.

Uchaguzi huo, uliotawaliwa na kashkashi za hapa na pale, ulifanyika katika ukumbi wa NSSF WATER FRONT, Dar es salaam
 
Jamal Malinzi ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha soka cha mkoa wa Kagera ameshinda uchaguzi huo ikiwa ni mara yake ya pili kugombea baada ya kushindwa na Rais wa zamani wa TFF Leodgar Chillah tenga mwaka 2008.




Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger