Asha Baraka Awavaa Mastaa wanaobadili Dini kwa ajili ya Pesa
Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka. |
MKURUGENZI wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’ ya jijini Dar, Asha Baraka amelivalia njuga suala la baadhi ya mastaa wa Kibongo kubadili dini kwa ajili ya kuwafuata wanaume au wanawake ili wajipatie fedha.
Asha alibainisha hayo hivi karibuni na kubainisha kwamba wapo wasanii wanaobadili dini kwa ajili ya kufuata fedha kwa wapenzi wao , pindi wapenzi hao wanapoishiwa wanajidai kurejea katika dini zao za awali.
“Binafsi nakerwa na tabia hizi za wasanii, ni heri mtu ubadili dini kwa imani ya kweli, siyo kwa ajili ya kufuata fedha, ni vibaya sana,” alisema Asha kwa masikitiko.
Hivi karibuni msanii Jacqueline Wolper alitangaza kurejea katika dini yake ya Ukristo baada ya kushauriwa na wazazi wake ingawaje watu wengine wamedai kwamba Wolper alifanya hivyo baada ya aliyekuwa mchumba wake Abdallah Mtoro ‘Dallas’ aliyemfuata kwenye Uislamu kuishiwa fedha.