Filamu ya KIGODORO ya Zamaradi Mketema, yamgharimu milioni 16
Mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds TV, Zamaradi Mketema hivi karibuni aliingia msituni kuandaa filamu yake iitwayo ‘Kigodoro’ iliyoshirikisha mastaa wakiwemo Hemedy PHD, Kajala na Muhogo Mchungu.
Akiongea na mwandishi wetu, Zamaradi alisema aliamua kuandaa filamu hiyo baada ya kuona kuwa filamu nyingi za Tanzania zina hadithi zile zile hivyo alitaka kuja na kitu tofauti.
“Tuna mambo mengi sana ambayo yanaendelea Tanzania ambayo yanaweza kukaa kwenye filamu yakachekesha, yakafurahisha, yakaelimisha. So nikafikiria, nikawaza yale maisha ya uswahilini, watu wanasutana, wanagombana, yale maisha ambayo unakuta chai ipo lakini vitafunio mnajitegemea, nimejaribu kuangaza familia ya aina ile,”alisema Zamaradi.
“Nikatoa idea, nikampa mtu aniandikie script, akaandika script vizuri ndo tukaingia mzigoni.”
Zamaradi amesema hadi sasa gharama aliyoitumia kutengeneza filamu hiyo ni zaidi ya shilingi milioni 16.