Pamoja na skendo ya kuibiana Mume, Jokate ajitokeza na kumfariji Wema Sepetu baada ya kufiwa na baba yake mzazi.
LICHA ya kuwa waliwahi kupokonyana bwana (Nasibu Abdul ‘Diamond’), mwigizaji Wema Sepetu na mtangazaji Jokate Mwegelo wamekutana katika msibani na kupiga stori.
Kwa mujibu wa meneja wa Wema, Martin Kadinda, Jokate aliibuka Jumanne iliyopita usiku kwenye msiba wa baba Wema uliochukua nafasi nyumbani kwao Sinza-Mori jijini Dar na kumfariji hadi usiku mnene.
“Fani ya urembo na ubunifu ni fani za watu makini sana ambao chuki kwao ni mwiko, nimefurahishwa na kitendo cha Jokate kuja msibani kwani anaonyesha dhahiri kuwa ni mtu mwenye huruma na imani,” alisema Kadinda.